Kuhusu Kamusi
Kamusi Hai ya Kiswahili Kwenye Mtandao ni mradi shirikishi wa watu kutoka kila sehemu duniani. Pamoja tunatengeneza kamusi mpya za Kiswahili, kwa Kiswahili chenyewe na baina ya Kiswahili na Kiingereza. Tunaandaa vitabu na matumizi kwenye kompyuta zinazopatikana kutoka ukurasa huu huu. Tunakukaribisha kuwa mtengenezaji mchangiaji - saidia kuboresha kamusi yetu kwa kutumia Chombo cha Untengenezaji. Kiswahili husemwa na watu wengi kuliko lugha zote za kiafrika. Wako zaidi ya watu hamsini milioni wanaosema Kiswahili. Twaomba wageni wapya wasome kwanza ukurasa wetu wa Maswali ya Kawaida.

Kazi ya Kamusi Hai ni sehemu ya Yale Program in African Language na Council on African Studies huko Yale, chini ya Yale Center for International and Area Studies.

« »

Faces of Africa, maonyesho ya picha maalum

Tunasaidiwa na Wasomaji Wetu
Mradi huu hupatikana bure kwa watumiaji wote. Ukiweza, twaomba utusaidia kuendeleza na kupanua rasilimali za mradi kwenye michango yako. Bonyeza hapa na fuata maelezo utakayosoma. Twakushukuru ukiweza kuchangia yoyote.

Habari zetu mpya - 2 Machi, 2005
Pakua programu bure za Kiswahili kutoka kompyuta yetu, kama Jambo OpenOffice na TuKsi Koti la Rangi. Programu mpya zinapatikana hapa. Tumieni na raha! Pia, hivi karibuni tumetambulisha uso mpya, tumeanzisha Chombo cha Wapigapicha, tumeboresha Utafutaji katika Kamusi, na tumegawa istilahi na lahaja mbalimbali katika Kamusi Hai. Sasa tunaanza kuandaa masomo kwa wanaotaka kujifunza Kiswahili - angalia hapa baadaye kwa habari zaidi.

Stockholm Challenge 2001 Mshindani Juu - soma zaidi
Kamusi Hai ilichaguliwa kuwa mshindani juu kwenye Stockholm Challenge 2001, mashindano ya kimataifa kwa miradi bunifu ya elimu na utamaduni, hufadhiliwa na Mji wa Stockholm, Sweden.

Vipengee Kugundua:


Hatimiliki
Kurasa zote za Kamusi Project zina Hatimiliki 1995-2005 Yale Program in African Languages

Asante kwa kutembelea Kamusi Project. Ukurasa wa kwanza wa Kamusi Project uliumbwa Aprili, 1995.


Home / Nyumbani  :::  Top / Juu