Zana ya Uhariri ya Kamusi Hai
Karibu kwenye Zana ya Uhariri ya Kamusi Hai. Chombo hiki ni zana muhimu inayokuwezesha kushiriki moja kwa moja kuendeleza Kamusi Hai. Wakaribishwa kutumia Zana ya Uhariri kuhariri maneno yaliyopo au kuongeza tafsiri mpya. Marekebisho au nyongeza yoyote utakayofanya yatapitiwa na Mhariri wa Kamusi Hai na kisha kuwekwa rasmi ndani ya Kamusi Hai inayoweza kutumiwa na watu popote walipo duniani.
Kabla ya kutumia Zana ya Uhariri, itabidi ujiandikishe kama mchangiaji wa Kamusi Hai.
Unaweza Kuhariri Kamusi Hai kwa Kufuata Hatua Tatu Rahisi
 |
Kwanza, fungua Zana ya Uhariri. Unaweza kutumia kisanduku kilichopo hapa chini (kitakachoanza kufanya kazi hivi karibuni) ili uweze kutafuta neno la kuhariri, au (kwa sasa) unaweza kufika kwenye Zana ya Uhariri kwa kubofya "[ edit entry ]" baada ya kila neno lililomo kwenye Kamusi Hai.
|
 |
Pili, bofya kitufe kilichoandikwa "Edit - Hariri" ili uweze kufanya mabadiliko kwenye maingizo uliyoyachagua kwenye kamusi. |
 |
Ukihitaji kuongeza mistari mingine, chagua nambari iliyo kandoni mwa "Mistari ya ziada iliyo wazi." |
 |
Fanya mabadiliko kadiri utakavyo, kisha uyapitie upya kwa kubofya "Onyesha mabadiliko". |
 |
Iwapo utaona vitu zaidi unavyohitaji kubadili, basi bofya "Fanya mabadiliko zaidi" na endelea kuhariri.
|
Tatu, bofya "Pitia kwa makini" ikiwa ni fursa ya mwisho ya kupitia upya mabadiliko uliyoyafanya. (Ikiwa wataka sasa kufanya mabadiliko mengine zaidi, itabidi ubofye kitufe-rejeshi cha kivinjari unachotumia.)
|
 |
Bofya "Tuma mabadiliko". Mabadiliko uliyofanya yatatumwa sasa kwenda kwa Mhariri kwa kupitiwa, na punde yatajumuishwa kwenye Kamusi Hai!
|
 |
Ukihitaji maelezo ya ziada kuhusu mchakato huu au eneodata, tazama orodha ifuatayo hapa chini.
Hariri sasa
Kama umeshatafuta kwenye Kamusi Hai kwa lugha zote mbili, na ukiwa na uhakika kwamba kuna neno ambalo halimo, unaweza kuweka neno hilo kwa namna ya kuchagua idadi ya mistari mipya unayotaka kuweka.
|
Maeneodata ya Zana ya Uhariri pamoja na maelekezo
Maelekezo ya ziada kuhusu unavyoweza kuhariri Kamusi Hai