The following discussion at sw.wikipedia.com (article TOGWA) needs some more knowledge. Basically: is togwa just some unalcoholic state of pombe before fermenation or something else?
I repost the following 5 entries:
1
Je kuna tofauti gani kati ya togwa na pombe la kawaida? Yaani pombe ya mahindi, ulezi na kadhalika? Ni aina tofauti au aina ya pekee au ni lugha ya eneo tu? --
2
Nadhani ni tofauti za kimaeneo. Lakini ngoja niulize watu wengine. --
Kumbe kamusi ya KKK/SED yasema: "togwa , native beer (pombe) in the sweet, unintoxicating state, not fermented". Kumbe ni kama divai changa kwenye nchi za Mediteranea ambayo ni zaidi kama maji ya mizabibu. --
3
Lakini katika Kamusi ya kiswahili sanifu yasema: Togwa ni kinywaji kisicholeyva kinachotengenezwa kwa kimea, unga wa mtama au ulezi na sukari. --
4
Basi naona ni ileile hakuna tofauti. Sijui togwa lakini kutokana na maelezo yako nadhani ya kwamba togwa itabadilika kuwa pombe isiponyewa yaani ikiachwa vile itaanza kuchachuka. Kweli? Au kuna mbinu inayozuia kuchachuka na kuwa na kiwango cha pombe ndani yake? --
Swahili Bookstore
Books, Music,
Movies, More!
Pour les francophones:
Le swahili simplifié
Most Recent Searches
Swahili to English
|
Sina la ziada ...
Kufuatana na marejeo yangu “togwa†ndio kinywaji baridi kisicholewesha cha mtama, unga na sukari. Haifanyi mtu kuwa keroro!
Hukata kiu mara moja kuliko maji baridi. Sina la kusema kuhusu hali yake kama hatua inayotangulia kufanyika kwa pombe yenyewe.
togwa ni pombe kabla ya kuwa pombe
Togwa ndiyo itakuwa pombe ikikaa. Kwa mfano, togwa ya ulanzi ni utomvu kutoka mianzi baada ya masaa kadhaa, na ulanzi wenye pombe ni utomvu uleule kutoka mianzi baada ya siku mbili hivi.
Asante, nimepokea ushauri
Asante, nimepokea ushauri huu hoja lako limo wikipedia sasa. (http://sw.wikipedia.org/wiki/Togwa)